Home Lifestyle A-BOYS WAKANUSHA KAULI YA AT KUHUSU UBAGUZI KWENYE MUZIKI

A-BOYS WAKANUSHA KAULI YA AT KUHUSU UBAGUZI KWENYE MUZIKI

Kundi la wasanii wa bongofleva kutoka Zanzibar A-boys wamekanusha uwepo wa ubaguzi wa wasanii kutoka Zanzibar kupewa sapoti katika #bongofleva Tanzania na kusema kuwa mfumo wa kijamii Zanzibar ndio chanzo cha kutokuwepo kwa wasanii wengi kwenye Tasnia hii.
Kauli hii inapingana na ile ya AT ambaye alinukuliwa akisema Mziki anaofanya unashindwa kutoboa vizuri kwasababu unabaniwa kwakuwa Asili yake ni Zanzibar. A-boys wamesema Zanzibar kwa miaka mingi imekaa ktk miongozo ya kidini sana kwahiyo Bongofleva au Mziki kiujumla ulichukuliwa kama uhuni.
Lakini sababu nyingine ni kwakuwa Tanzania Bara kuna nguvu kubwa ya #Media ukilinganisha na kule visiwani. Amesema Badi sky kutoka A-ABOYS.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here