Home Lifestyle Afya Ya Chid Benz Yazidi Kuzorota ! (Picha)

Afya Ya Chid Benz Yazidi Kuzorota ! (Picha)

Hiyo jana picha zilisambaa sana  katika mitandao ya kijamii zikionyesha kuzorota kwa afya ya msanii mkongwe wa Bongo Chid Benz akiwa amepungua mwili na kuonekana ni dhaifu, jambo ambalo limewahuzunisha mashabiki wengi.Kwa upande wake msanii Afande Sele alipost picha hiyo ya Chid Benz na kusema madawa ya kulevya ndiyo chanzo cha kudhoofika kwa afya ya chidi, Afande alisema kwamba madawa ya kulevya yanaua vijana na  kusisitiza kwamba hayaleti maendeleo yoyote bali ni  kupoteza vijana ambao ndio nguvu  ya taifa . “Yanapita kwa njia gani madawa ya kulevya hapa nchini? anayasambaza nani mitaani kote? madawa ya kulevya hayaleti maendeleo, madawa ya kulevya yanaua masela leo” Alisema Afande Sele.

IMG_2050

Ni siku chache tu   Chid Benz akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio  ambapo alisema kwamba kwa sasa  anatambua alipotoka na sasa yupo katika harakati za kujirekebisha.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here