Home Lifestyle AY Azungumzia Kufungiwa Kwa Video Yake Ya ZIGO

AY Azungumzia Kufungiwa Kwa Video Yake Ya ZIGO

Rapper Ambwene Yessayah aka AY, amesema kuna video nyingi ambazo hazijazingatia maadili wala maudhui bado zinaendelea kuonyeshwa kwenye TV. Siku chache zilizopita msanii AY alipost picha ikimuonyesha akiwa yupo na maafisa wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA akiwa ameenda kutafuta muafaka juu ya kufungiwa kwa video yake ya “Zigo Remix” ambayo bado inaendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa youtube ikiwa imeshapata viewers zaidi ya milioni tatu.

AY1
Akiongea na Mkasi TV, wakati wa kikao hicho AY alisema, “Nashangaa kufungiwa kwa video yangu wakati kuna video nyingi bado zinaendelea kuonyeshwa kwenye vituo vya TV, kwa mfano video ya Anaconda. Huwa narekodi saa hadi dakika za baadhi ya video hizo zinaporuka.”
“Tumekubaliana nirekebishe baadhi ya vitu kwenye video yangu baada ya hapo wakiidhinisha itaendelea kuruka tena kuanzia asubuhi siyo mchana tu,” aliongezea AY.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here