Home Lifestyle Baada Ya Kupata Umaarufu Huo Wote,Bado Harmonize Aishi Kwa shida.

Baada Ya Kupata Umaarufu Huo Wote,Bado Harmonize Aishi Kwa shida.

Msanii huyu ambaye alikuletea kibao cha Bado na Diamond platinumz amepata umaarufu mkubwa baada ya kukitoakibao hiki.Lakini wengi hawafamu siri iliyopo katika lebo ya WCB inayomilikwa na Diamond platinumz, Harmonize amesema kwamba scandle mingi chafu huwafuata lakini hawana budi kufuata nyayo za boss wao Diamond ili Kuwa na picha nzuri katika Jamii.

Harmonize-3

Harmonize katika mahojiano na Radio Ya East African Radio amesema kwamba  wao kama WCB hawana kawaida ya kwenda club kutokana na kubanwa na majukumu shida ambazo alisema wanazipitia kwa sasa.Aliongezea kwamba hali hiyo imemsaidia mkubwa wao Diamond kuteka anga za East Afrika Kimziki.

”Labda nizungumze kitu kimoja, WCB sio mimi tu hata wasanii wengine ambao watatoka WCB kuna life style ambayo watafuata, lakini mimi kama mimi sipajui club kabisa, sijawahi kwenda club sitokagi, kwa sababu pale ofisini kuna studio studio mle mle ndani, kuna vyumba ambavyo ukirekodi ukichoka unakaa unarefresh mind, kuna game station mnakaa mnacheza game, alafu pia kuna vyumba vya kuishi mule mule, muda wenyewe wa kutoka unakosa, alafu pia ukizingatia CEO mwenyewe wa WCB hana hizo mambo za kwenda club, so sisi tunajifunza kupitia yeye”, alisema Harmonize.’

Harmonize pia aliongezea kwamba umaarufu alioupata kwa sasa unamzuia kutembelea maeneo aliyokuwa amezoea kitambo  pia kujihusisha na wasanii mbalimbali ili kujiepusha na scandle amabazo mara wa kadha huwakumba wasanii wengi.

“Juzi kulikuwa na mwaliko Mh Rais alialika wasanii Ikulu, mi sikuenda kwa sababu sijazoea hayo mazingira, kwa hiyo inakuwa ngumu kuhusishwa na skendo huyo mwanamke nakutana nae wapi, sababu muda wa kutoka nakuwa sina, mi sikutanagi na wasanii wenzangu yani, muda naukosa kabisa, na ndo kati ya vitu ambavyo navimisi kabisa”, alisema Harmonize

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here