Home Lifestyle “Baba Yangu Alifungwa Nikiwa Tumboni” -Ben Pol

“Baba Yangu Alifungwa Nikiwa Tumboni” -Ben Pol

Msanii Ben Pol ambaye hivi majuzi ameachia kazi yake mpya ‘Moyo Mashine’ amefunguka na kusema kuwa Baba yake mzazi alifungwa kifungo cha miaka miwili wakati mama yake mzazi akiwa na ujauzito wake. Ben Pol amesema hayo kupitia kipindi cha 5 Selekt kinachorushwa na EATV na kudai kuwa licha ya baba yake kufungwa lakini Mama yake mzazi alipigana mwanzo mwisho kwa kuuza maandazi na vitumbua mpaka alipozaliwa na kumpa malezi. “Unajua mimi najua nilipotoka mpaka nilipofika hapa naweza kusema I made it, wakati mama yangu ana ujauzito wangu wa miezi sita baba yangu mzazi alifungwa jela miaka miwili hivyo mama alipambana kwa kuuza maandazi na vitumbua mpaka nazaliwa na kunilea hivyo leo kwa hapa nilipofika huwa napenda kushare historia yangu ili watu wajue,” alisema Ben Pol. Mbali na hilo Ben Pol anasema kuwa yeye hakuzaliwa hospitali bali mama yake mzazi wakati wa kumzaa yeye alijifungua akiwa nyumbani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here