BABU TALE Adai Alidhani CHIDI BENZ ana Ukimwi

  Meneja wa Diamond na kundi la Tip Top Connection, Hamisi Taletale ‘Babutale’ amedai kuwa alipoziona picha za Chidi Benz kwa mara ya kwanza alidhani msanii huyo ameambukizwa virusi vya Ukimwi.
  Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatano hii, Babutale amesema kwa muonekano aliomuona nao Chidi Benz hasa zaidi kwenye picha ambazo zilikuwa zikisambazwa kwenye mitando ya kijamii zilimtisha na kuhisi labda Chidi Benz anasumbuliwa na maradhi mengine kama ngoma.

  Chidi Benz
  “Kusema ukweli nilipoona picha ile nilipata wasiwasi nikidhani Chidi Benz labda ameungua na maradhi yetu ya sasa, sikuamini kama ni madawa ya kulevya ndiyo yamempelekea hali ile. Lakini sikuweza kuamini kesho yake ilibidi nimchukue Chid Benzi na kwenda nae kwenye kituo cha afya na kufanya check up ya mwili mzima, lakini baada ya vipimo kutoka akaonekana yuko poa kabisa ila wakagundua tu ni hayo madawa” alisema Babutale.
  Babutale, Chidi Benz na Kalapina wakiwa Bagamoyo Sober House
  Katika hatua nyingine Babu tale amesema yeye aliamua kumsaidia Chid Benzi ili aweze kurudia katika hali yake ya kawaida na aendelee na maisha yake ya kawaida na si kusema ameamua kumsaidia kwa sababu ya kutafuta kiki au kutafuta maslahi kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidai.
  Chidi Benz kwa sasa yupo Bagamoyo Sober House akisaidiwa kuacha matumizi ya Madawa ya kulevya.

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here