Home Lifestyle Babutale Aeleza Mipango Waliyonayo na Hakeem wa Empire…

Babutale Aeleza Mipango Waliyonayo na Hakeem wa Empire…

Diamond Platnumz na meneja wake Babu Tale wanajitahidi kutumia kila fursa inayokua mbele yao. Hivi karibuni wawili hao walikutana na mwigizaji maarufu wa Series ya ‘Empire’  Yazz anayejulikana Zaidi kama ‘Hakeem’  jijini Los Angels, Marekani.

Kupitia kipindi cha Playist cha Times Fm, Babutale alieleza jinsi walivyokutana na msanii huyo na kilichofuata baada ya hapo.

“Jamaa ‘Yazz’ alikuja kwenye hoteli tuliofikia na alikuwa na mambo yake. Mimi sijuagi zile movie nisiwe muongo, nimemuona tu hivi akina Diamond anaongea nae. Mchana nimeona mabango yake mji mzima, LA nzima imechafua Billboard, kwahiyo nikamkumbuka huyu nimemuona mchana, baada ya kumuona kila niliporudi ilibidi niangalie Empire vizuri. Pale tulipokuwa tunaongea nae, tunachange namba,  tukamwambia sisi tunatokea Africa, akesema, “I wish to be in Africa”, nikamwelezea huyu ni msanii wangu mkubwa, baada ya kuangalia profile ya Diamond akawaka vile. Haijaishia hapo tukabadilishana na namba, na mchizi anatamani kuja hata Bongo anytime. Tunachat nae kidogo, soon tunaenda Marekani kuna kitu tunaenda kufanya najua tutakutana nae na tutamaliza maongezi yetu na  hauwezi jua labda mwaka huu tunaweza tukamwalika”, alisema BabuTale.

 

Courtsey: Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here