Home Lifestyle BEKA Atoa Sababu Ya Kurudia ‘Aje’ ya ALIKIBA

BEKA Atoa Sababu Ya Kurudia ‘Aje’ ya ALIKIBA

Msanii Beka Ibrozama amefunguka sababu ya kufanya cover nyimbo ya ALIKIBA #Aje. Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Beka amesema swala hilo ni jambo ambalo haliwezekani kwani yeye tayari yupo kwenye uongozi, ambao unamsimamia kazi zake. “Suala la kuwa tayari Kusa signiwa na Alikiba haiwezekani kwa sababu mi nipo kwenye management ambayo nina mkataba nayo, management ambayo imeninulia vifaa vya bendi, na sasa hivi ndani ya miezi hii mitatu au minne mbele nitazindua bendi yangu”, alisema Beka. Pia Beka amesema yeye ameamua kufanya hivyo kwani ni wimbo amabo anaupenda na pia ni shabiki mkubwa wa Alikiba, hivyo ameamua kumpa ushirikiano msanii huyo.
“Kufanya ngoma ya Alikiba mimi ni shabiki wa Alikiba, naipenda na nyimbo ya Alikiba ndio maana nikaamua niimbe kwa feelings zangu lakini kutumia maneno yake, na pia napenda usapoti vya nyumbani kwa hiyo nikaona nimsapoti brother”, alimalizia Beka.

Eatv

4 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here