Home Lifestyle Belle 9 Asema Wasanii Kushoot Video Nje kunawafanya wajifunze Vitu Vipya

Belle 9 Asema Wasanii Kushoot Video Nje kunawafanya wajifunze Vitu Vipya

Msanii wa muziki wa R&B Belle 9 amesema wasanii wanaenda kushoot video na directors wa nje ili kujifunza na kutanua wigo wa muziki wako.
Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Belle 9 amesema wasanii kwenda kushoot video nje kunawafanya wanjenge connection mpya.
“Kwenda kushoot nje ya nchi ni exposure, kwa sababu ni kama umetoka Morogoro unafanya kolabo na msanii wa Arusha, sehemu ambayo unatoka na sehemu unayoenda ni ugenini always utaongeza kitu tu. Kwa sababu kuna watu wengine wana njia nyingine za kufanya kazi na biashara. Kwahiyo muziki ni lugha ambayo popote inaeleweka, haina tabaka,” alisema Belle 9.
Aliongeza, “Kwahiyo ni kitu kizuri sana kolabo za nje pamoja na kufanya kazi na watu tofauti, hata kushoot video. Hapa ndani pia tuna directors wazuri, wasanii wazuri, pia kuna wadau wazuri ambao wanaweza kuwafikisha wasanii sehemu. Tumeona wasanii wengi miaka hii ya karibuni wametusua kutokana na kujichanganya na kutojiwekea mipaka ya kufanya kazi,”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here