Home Lifestyle Ben Pol Adai Collabo Yake na Nameless iliyovuja Imeharibu Mipango Ya Moyo...

Ben Pol Adai Collabo Yake na Nameless iliyovuja Imeharibu Mipango Ya Moyo Mashine

King of R&B Bongo, Ben Pol amedai kuwa hajui la kufanya baada ya wimbo wake wa ‘Yamenikuta’ aliomshirikisha msanii wa Kenya, Nameless kuvuja na kuharibu baadhi ya mipango yake.
Wimbo huo umevuja mapema mwezi Agosti mwaka huu na umetayarishwa na Sappy kutoka nchini Kenya. Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha E News cha East Africa TV, “Kwanza ile ngoma haijatoka kwangu wala kwa Nameless, producer pia tumemuuliza amesema haujatoka kwake lakini ngoma ipo kwenye mitandao.”
“Mimi sijawahi kuipost popote, kwahiyo tunawaza tu. Tupo kwenye kigroup cha Whatsapp tunawaza tufanyaje maana wimbo kila mtu anao. Tunaangalia tufanyaje aidha tushoot video au tulaunch na mgeni rasmi,” ameongeza. Aidha msanii huyo amedai kuwa kuvuja kwa wimbo huo kumemuathiri sana mipango yake kwa kuwa bado alikuwa anafanya promosheni ya wimbo wake Moyo Mashine huku akijipanga kuachia remix ya wimbo huo aliomshirikisha Chidinma wa Nigeria.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here