Home Lifestyle Bob Junior Aweka Wazi Kwanini Video Yake Na Chameleone Haijatoka

Bob Junior Aweka Wazi Kwanini Video Yake Na Chameleone Haijatoka

Producer na muimbaji wa Bongo flava Bob Junior, amefunguka kwanini video ya wimbo aliyofanya na mkali tokea pande za Uganda, Jose Chameleone bado haijatoka. Bob Junior alidai kuwa alikuwa na nia ya kufanya video ya wimbo huo lakini kila alipokuwa anapanga ratiba za ku’shoot, Chameleone alikuwa akikwepa. Akipiga story na eNewz Bob Junior alisema “Tukipanga siku ya ku’shoot, ikifika siku hiyo nikimtafuta basi hajibu meseji zangu, sasa mimi nitafanyaje? Hata hivyo sitaki kusema mengi kwa ubaya, labda kuna vitu kweli vinamzuia”. Hata hivyo Bob Junior alisema baada ya kushindwa kufanikisha kufanya video hiyo, sasa anajipanga kwa kazi nyingine, huku akisema anatarajia kuachia wimbo alioshirikiana na Q Chief na Baraka da Prince, wimbo unaoitwa “Kidege” na kama si wimbo huo basi ataachia mwengine unaoitwa “Mpasuo”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here