Home Lifestyle Chidi Benz Adai Babutale Ameshatumia Zaidi Ya Milioni 40 kwaajili Yake

Chidi Benz Adai Babutale Ameshatumia Zaidi Ya Milioni 40 kwaajili Yake

Kwa Chidi Benz, Babutale ni mtu mwenye umuhimu wa aina yake na atamheshimu daima kwasababu meneja huyo wa Diamond ametumia fedha nyingi hadi sasa kwaajili yake. “Huwezi amini mpaka sasa hivi ninavyoestimate kwamba Tale anaweza akawa ametumia kama milioni 45, 50, 60. Sio kuwekeza, vitu ambavyo vimefanyika tayari, lakini sijasaini wala nini,” alisema Chidi kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM. “Tale anachokifanya anaonesha kwamba ‘nia yangu mimi sio lazima tukabane kwenye suala la hela, nia yangu wewe uwe sawa, uwe okay, uwe poa.’ Kwahiyo ina maana mimi sijasaini lakini nachukulia kwamba yeye aone kusaini inawekana nikasaini ukaniletea mkataba wa miaka miwili but mimi sasa naishi na wewe kabisa,” aliongeza. Chidi anadai kuwa anamchukulia Tale kama familia yake.
“Kwasababu hata sasa hivi nakaa kwake, bado niko kwao so yaani kwahiyo hata ukija mkataba labda aniandikie miaka 20 kwamba haina maana.” Tale alimsaidia rapper huyo kumsaidia kuepukana na uraibu wa madawa ya kulevya ikiwa pamoja na kumpeleka rehab na baada ya kutoka kuingia studio kurekodi nyimbo mpya. Hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya ‘Chuma’ aliomshirikisha Raymond.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here