Home Lifestyle “Chumba Cha Video Ya ‘Matatizo’ Ndicho Nilichokuwa Nimepanga”- HARMONIZE

“Chumba Cha Video Ya ‘Matatizo’ Ndicho Nilichokuwa Nimepanga”- HARMONIZE

Harmonize amefafanua kuwa chumba kinachoonekana kwenye video ya ‘Matatizo’ ndicho chumba chake alichokuwa anakaa huko Kiwalani kabla hajawa staa. Akiongea na Magic FM Jumanne hii, Harmonize alisema kuwa kuimba nyimbo za matatizo uliyowahi kupitia zinasaidia kuwa inspire watu japo wengine wanadai kuwa kufanya hivyo ni ushamba.
“Muda mwingine kueleza matatizo uliyoyapitia ni kama ushamba hivi, muda mwingine kueleza vitu ulivyopitia ni kitu kizuri kwa kuwa unawa inspire vijana wengi sana ambao wapo mtaani hata wazee pia waliokaribia kukata tamaa,” alisema Harmonize.
“Kwenye video ya matatizo kwa asilimia kubwa vyote nilivyoimba ni historia yangu kabisa. Hata kile chumba nilichoshoot video ndio chumba nilichokuwa nimepanga wakati nakaa Kiwalani,” aliongeza.
Aidha Harmonize aliongeza kuwa wakati anakaa kwenye chumba hicho aliweka kapeti lake la bei rahisi na kigodoro pekee.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here