Home Lifestyle “Dawa za kulevya zitatutenga Wasanii na Jamii “- Asema AY

“Dawa za kulevya zitatutenga Wasanii na Jamii “- Asema AY

Msanii wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’, amesema kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini kutashusha soko la wasanii hao kwa kukosa uaminifu. “Mimi binafsi nashindwa kuelewa kwanini wasanii wanajitumbukiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na huko tunakoelekea tutashindwa kuaminika kwa jamii, familia zetu hata kwa watoto na marafiki, inabidi tupigane kwa pamoja, huku tukimshirikisha Mungu atuepushe na hayo mambo,” alisema AY.
AY aliongeza kwa kuwa muziki wa kizazi kipya kwa sasa una nafasi kubwa, wasanii watumie fursa hiyo kujiendeleza kimuziki kwa kushirikiana na wasanii wa mataifa mbalimbali, ili kukuza uchumi badala ya kushirikiana katika matumizi ya dawa za kulevya. “Kinachotakiwa kwa sasa, wasanii watumie fursa za kushirikiana na wasanii wenye mashabki wengi kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kujiongezea mtandao, soko na fedha zaidi, siyo kujiingiza katika matumizi au uuzaji wa dawa za kulevya,’’ alifafanua AY.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here