Home Lifestyle DEFAO Azuiwa kwa Kushindwa kulipa bili ya hoteli Mombasa, JAGUAR Ajitolea Kumlipia

DEFAO Azuiwa kwa Kushindwa kulipa bili ya hoteli Mombasa, JAGUAR Ajitolea Kumlipia

Muimbaji wa Kenya, Charles Njagua Kanyi, maarufu kama Jaguar, alijitokeza kusaidia kulipa deni alilokuwa akidaiwa muimbaji mkongwe wa DRC, Defao kwenye hoteli ya Mombasa, Kenya alikokuwa ameshikiliwa Jumamosi.
Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 57 alikuwa ameshikiliwa kwenye hoteli ya Rickseaside Villas huko Nyali kwa kushindwa kulipia gharama za chakula na malazi.“Kutokana na tukio hilo la bahati mbaya la General Defao, aliyeshindwa kulipa bili kwenye hoteli ya Mombasa, nimejitolea kulipa kiasi hicho cha fedha kwakuwa mimi ni msanii kama yeye na hiyo inaweza kutokea kwa yeyote,” alisema Jaguar.
Muimbaji huyo alikuwa anadaiwa shilingi 20,000 za Kenya ambazo ni takriban shilingi 360,000 za Tanzania. Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa klabu ya Mombasa ilikataa kulipa bili hiyo. Alidai kuwa uongozi wa klabu hiyo uliompeleka Mombasa, ulimtaka akae na kutumbuiza, August 3 lakini hakutumbuiza. Bili ya kuanzia July 28 hadi August 1 ilikuwa imelipwa tayari lakini klabu hiyo ilikataa kulipia siku 4 zilizoongezeka. Defao alikuwa Mombasa kwenye show mwishoni mwa wiki.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here