Diamond Platnumz Aunga Mkono Kutozwa Milioni 10 Plate Namba

    Msanii wa Bongo Flava Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz amesema anaunga mkono kitendo cha serikali kutangaza kwamba kwa watu wanaotumia plate number za majina yao watatozwa milioni 10 kama kodi kutoka 5 kuanzia mwaka wa fedha 2016 & 2017. Kufuatia hotuba ya serikali kuonyesha hivyo kipindi cha EA DRIVE kinachorushwa na EA Radio kimeongea na msanii Diamond Platnumz kuhusu mkakati huo ikiwa yeye ni mmoja wa wanaolengwa na jambo hilo.
    Akijibu swali hilo msanii huyo amesema mtu anayetaka kuweka Plate Number ya jina lake maana yake anafedha zilizokithiri na kama anafedha zilizokithiri bora serikali ichukue fedha hizo ikasaidie watu wengine. ‘’Kama serikali itatumia fedha hizo kusaidia watu wa hali ya chini, mimi naona sawa tuu’’ amesema Diamond.

    LEAVE A REPLY

    Please enter your comment!
    Please enter your name here