Home Lifestyle FID Q :MSIMCHEKE CHID BENZ NI MAPITO TU

FID Q :MSIMCHEKE CHID BENZ NI MAPITO TU

Rapper Mkali kutoka Mwanzo Fareed Kubanda Ukipenda FID Q amesema Chid Benz ni Mmoja ya Wasanii wa Hip Hop ambaye anamkubali sana na yale yaliyomtokea siyo mambo ya kufurahia ila ni kumsapoti pale tunapohitajika kufanya hivyo ili aweze kurejea kwenye game. Juzi kulikuwa na mjadala kuhusu kauli ya Chid Benz kusema Rapa kutoka Morogoro STAMINA alikuwa anamkubali sana yeye na siyo Fid Q kama inavyoonekana jambo ambalo stamina alikuja kulikanusha. Kuhusu hilo FID hakutaka kulizungumzia sana lakini amesema issue za CHID BENZ kupotea kwa kile kinachosemwa ni matumizi ya #Unga bado hakiondoi ukweli kwamba bado kipaji chake kipo pale pale. Ameongeza kuwa CHID benz mpaka sasa hivi ni rapa ambaye anaweza kumualika wakafanya show pamoja na anaamini bado uwezo anao kwasababu kipaji hakipotei.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here