Home Lifestyle H_Art The Band Wanusurika Kifo

H_Art The Band Wanusurika Kifo

Kundi la wasanii Wa Muziki wa Humu Nchini H_art The Band, wamenusurika ajali mbaya iliyotokea Jana asubuhi.
Katika ukurasa wao wa instagram wasanii hao wamepost picha ya gari ambalo walikuwa wanatumia, huku wakiandika ujumbe wa kumshukuru Mungu kwa kuwanusuru kwa ajali hiyo.

Hart.
“Truly, God is our Healer & Our Protector. This morning we got into a grisly accident & we Thank the Lord that none of us got seriously injured but one thing for sure is, for that split second just as we thought it was our last God rescued us & reminded us that truly, if the Lord is With You then nothing can harm you. We maybe in pain but don’t worry, we are OK *sisi ni maninja, we will survive*. Thank you all who put us in your Prayers Daily they keeps us going through our day., may the Lord Bless you #JahBles”.
Waliandika wasanii hao wakimaanisha…….(Mungu kweli ndiye mponyaji wetu na mlinzi, asubuhi hii tulipata ajali mbaya na tunamshukuru Mungu kwani hakuna hata mmoja wetu aliyepata majeraha makubwa, jambo moja kwa hakika kwa ule mgawanyiko wa pili ndiyo ulikuwa wa mwisho Mungu kutuokoa na kutukumbusha kuwa kweli ukiwa na Mungu upande wako, hakuna kitakachokudhuru. Tunaweza kuwa kwenye maumivu lakini msijali, sisi ni maninja, tutaishi. Ahsanteni kwa wote ambao mnatuombea, maombi yenu yanatufanya tuzipitie siku zetu, Mungu awabariki)
Wasanii hao ambao wametamba sana na kibao chao cha uliza kiatu na Nikikutazama, kwa sasa wako kwenye ziara ya kimuziki kutangaza wimbo wao mpya wa Baby Love.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here