Home Lifestyle HARMONIZE Asema Anaweza Kufanya Kazi na ALI KIBA , Amsifia

HARMONIZE Asema Anaweza Kufanya Kazi na ALI KIBA , Amsifia

Msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya WCB, Harmonize amesema yupo tayari kufanya kazi na Ali Kiba endapo ikitokea nafasi.
Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds FM Ijumaa hii, Harmonize aliulizwa kama anaweza kufanya kazi na Ali Kiba kama ikitokea nafasi.

Harmonize - Kasuku
“Unajua Ali Kiba ni msanii wa Kitanzania, ni msanii mzuri pia, so kolabo ikiwa na tija nitafanya naye kwanini nisifanye naye. Sio Ali Kiba tu, msanii yeyote wa Kitanzania,” alisema Harmozine.
Pia Harmonize alisema bado hajui kama kweli kuna beef kati ya Diamond na Ali Kiba.
“Mimi sijui kiukweli kama kuna beef, kwa sababu sijawai kukaa na Diamond siku moja akaanza kuongelea msanii mwingine tofauti. Diamond ni mmoja kati ya watu wanaosupport muziki wa Tanzania, ukiona kolabo nyingi za Tanzania na wasanii wa nje Diamond ana mchango wake,” alisema Harmonize. Kwa sasa Harmonize anafanya vizuri na video yake mpya ya wimbo ‘Bado’ aliyomshirikisha bosi wake Diamond.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here