Home Lifestyle Harmonize Asema Bado Hajaingia Kwenye Mahusiano ya Mapenzi , Aeleza Ni Kwanini

Harmonize Asema Bado Hajaingia Kwenye Mahusiano ya Mapenzi , Aeleza Ni Kwanini

Msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya WCB, Harmonize amesema anaona bado wakati wake sahihi wa kuingia kwenye mahusiano. Muimbaji huyo ambaye ameachia video ya wimbo ‘Bado’ hivi karibuni akiwa amemshirikisha bosi wake Diamond, amekiambia kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii kuwa bado ana tafuta mtu sahihi katika maisha yake. “Mimi bado sijaingia katika mahusiano,” alisema Harmonize huku akicheka.

Harmonize - Kasuku

Aliongeza, “Toka nimeingia kwenye utu uzima sijaingia kwenye mahusiano kwa sababu nataka nifanye maamuzi sahihi. Kwa sababu nataka nikiingia kwenye mahusihano niweke wazi kabisa kila mtu ajue. Unajua mtu ukiwa nae kwenye mahusiano alafu ukamficha ni dharau, mwanamke ambae anatunza usingizi wako, anakushauri kwanini usimweke hadharani, nikiwa kwenye mahusiano nitaweka wazi huyu ndiye wangu,” Pia Harmonize alidai mazingira aliyokulia yeye ni mazingira ambayo yanawafanya vijana wengi kuitumia starehe ya kufanya mapenzi kama starehe yao kubwa.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here