Home Lifestyle “Hata Ukisema Nije Kuimbia Kuku Ambao Hawatagi Nakuja”- Peter Msechu

“Hata Ukisema Nije Kuimbia Kuku Ambao Hawatagi Nakuja”- Peter Msechu

Msanii Peter Msechu ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa ‘ Mama’ ambao ni wimbo wa kushirikiana kati yake na Banana Zoro , Msechu amesema kuwa yeye pamoja na Banana Zoro hawachagui show hata ukitaka kuwaita waje kuimbia kuku wako ambo hawatagi ili watage wao watakuja cha msingi wao wanaingiza pesa . Akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo Peter Msechu alisema kuwa amejifunza kuwa katika maisha ya kila siku ukifanya jambo lako na kumgusa mwanamke au mama hilo jambo lazima litafanikiwa.
” Yanii sisi saizi hata ukija ukiniambia Msechu tunahitaji Band yako ije iimbie kuku wetu ambao hawatagi ili watage sisi tunakuja tunafanya yetu , maana kama daktari amekwambia hao kuku hawatagi mpka waimbiwe sisi tunaimba tu” alisema Peter Msechu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here