Home Lifestyle Hawa Ndiyo Wasanii Wa Tanzania Ambao DIAMOND PLATNUMZ Amewahi Kuwalipa ili Afanye...

Hawa Ndiyo Wasanii Wa Tanzania Ambao DIAMOND PLATNUMZ Amewahi Kuwalipa ili Afanye Nao Kazi

Msanii Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa kabla ya yeye kutoka kimuziki kuna wasanii watatu wakubwa aliwalipa pesa ili afanye nao kazi katika kutafuta yeye kutoka kimuziki. Diamond ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema alishawahi kumlipa Mr Blue elfu sitini, marehemu Albert Mangwea alimlipa shilingi elfu hamsini pamoja na Fatma mdogo wake na msanii Hard Mad. “Kabla sijatoka niliwahi kuwalipa wasanii wakubwa kipindi hicho ili nifanye nao kazi, niliwahi kumlipa Mr Blue, Albert Mangwea pamoja na Fatma, lakini kati ya wote hao msanii Chid Benz Chuma huyu jamaa yeye kwanza hakuwahi kunisumbua kwenye collabo, lakini pia hakunilipisha hata kumi, yaani sikuamini kabisa vile nilivyokuwa namsikia na nilipompigia simu na alivyonipokea ilikuwa tofauti sana” alisema Diamond Platnumz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here