Home Lifestyle Huenda ALI KIBA Akawa Kwenye Mpira Wa Kulipwa , Klabu Zaanza Kufanya...

Huenda ALI KIBA Akawa Kwenye Mpira Wa Kulipwa , Klabu Zaanza Kufanya Mpango Wa Kumsajili

Staa wa muziki, Ali Kiba amefunguka kuhusu suala la yeye kuingia kwenye soka ambapo amesema kuna klabu zimeanza kufanya naye mazungumzo. Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, Ali Kiba amesema kuwa hivi karibuni kuna timu ya mpira imemfuata kumtaka kujiunga na timu hiyo, lakini atakuwa na masharti ya kujiunga, kwa sababu bado anaupa kipaumbele muziki kuliko mpira. “Nitakuwa na condition zangu katika mpira kwa sababu muziki kwanza,” alisema Ali Kiba “Kuna timu imenifuata hivi karibuni, lakini nahitaji ‘ufree’ ambao hauwezi kunibana, nikiamua nina nafasi nafanya mpira,”
Aliongeza, “Unajua siku hizi promotion ni kitu cha msingi sana, niko na fans wengi sana kwa hivyo kuna watu ambao wananifuatilia wanaangalia either wanaweza wakawa mafans wa timu ambayo nitaenda kuchezea, kwa sababu najua mimi naenda kucheza sio kwa kucheza tu, kutakuwa na vitu vingi kwa hiyo watapata faida ya vitu vingi, watauza jezi na vitu kama hivyo”,

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here