Home Lifestyle Huyu Ndiye Msanii Wa Kwanza Afrika Mashariki kufanya Kazi Na JUSTIN CAMPOS

Huyu Ndiye Msanii Wa Kwanza Afrika Mashariki kufanya Kazi Na JUSTIN CAMPOS

Msanii wa Bongo wa Bongo Lady JayDee ameweka bayana kwamba yeye ni msanii wa kwanza Tanzania kufanya kazi na ‘director’ Justin Campos wa Afrika Kusini. JayDee ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa video yake ya NdiNdiNdi video ambayo imezinduliwa kwa mfumo wa kuitangaza na kuimba ‘live’ katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV.
“Nilikutana na Justin Campos kwa mara ya kwanza 2006 wakati tunafanya video ya ‘Njalo’ nilioshirikiana na kundi la Afrika Kusini linalojulikana kama ‘Mina Nawe’, Justin ndio alikuwa Director wa video hiyo baada ya miaka 10 tumefanyanae kazi tena 2016,” amesema Jaydee.
Video hiyo imezinduliwa huku msanii huyo akionyesha kweli kwamba yeye ni komandooo baada ya kupata mashabiki wengi ambao walikuwa wakituma pongezi na maswali kujibiwa katika kipindi hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here