“Jay Z Alifurahi Kukutana Na Mimi” – PREZZO

    Kupitia kipindi cha eNEWS Prezzo anasema yeye haitaji collabo za wasanii kutoka Afrika ili kutoka kimuziki sababu anajiamini na anajua anachokifanya na kusema kwamba wasanii wanatakiwa watambue kuwa yeye ameshawahi kukutana na msanii Jay Z na Jay Z alifurahi sana kukutana naye. “Mimi niko tofauti hivyo sifikiri nahitaji kufanya collabo na msanii wa nje ili nitoke, mimi najiamini sana lakini kumbukeni kwanza nilishakutana na Jay Z. Kwa hiyo nyinyi mnafanya collabo sijui na wasanii kama kina Davido mnaona mmefika mimi sipendi hicho. Jay Z alipokutana na mimi jamaa alifurahi kinoma yaani” alisema Prezzo. Msanii Prezzo amekuwa na tofauti kwenye muziki na msanii mwenzake JAGUAR japo kupitia eNews Prezzo alimpa shavu msanii huyo kwa kuweza kufanya collabo na Mafikizolo.

    LEAVE A REPLY

    Please enter your comment!
    Please enter your name here