Home Lifestyle Je! Chidi Benz Naye Kujiunga Na Label ya WASAFI?

Je! Chidi Benz Naye Kujiunga Na Label ya WASAFI?

Return of the King Kong. Baada ya kukosekana kwenye muziki kwa kipindi kirefu, msanii wa Hip Hop Bongo, Chidi Benz amerejea tena machoni mwa watu na muonekano mpya. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Chidi Benz amepost picha alizopiga kwenye studio ya WCB zinazomuonyesha akiwa na Diamond, Babu Tale na Harmonize hali inayozua shaka kuwa huenda King Kong akawa ameshamwaga wino wa kujiunga kwenye lebo hiyo ili kurudisha makali yake kama zamani. Aidha inadaiwa kuwa tayari Chidi ameshapika ngoma ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni japo bado haijajulikana iwapo wimbo huo umefanyika chini ya menejimenti ya WCB au laah.

Kila la kheri King Kong aka Chuma, nafasi yako kwenye muziki bado ipo.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here