Je Diamond Ana Beef Na Ommy Dimpoz?

  Msanii Diamond Platnumz amesema hana bifu na msanii wa bongo fleva Ommy Dimpoz. Katika mahojiano yake na Millard Ayo, amesema kwamba yeye na Ommy Dimpoz hawana bifu la aina yeyote, sema tu kuna ukaribu kidogo umepungua.

  “Mimi na Ommy Dimpoz hatujagombana sema kuna ukaribu kidogo tu umepungua.Amefika kwenye sehemu nzuri sasa ni wajibu wangu kuwashika wengine mkono wafanye kitu kizuri na yeye aweze kuwashika watu wengine. Tukishikana sisi wenyewe kwa wenyewe tutakuwa wabinafsi, hatuwezi kukua na kuwasaidia watu wengine,” Diamond alisema.

  “Mimi kwa sasa niko na Harmonize na Raymond”, aliongeza Diamond. Diamond Platnumz alisema kuwa ukaribu wake na Ommy umepungua kwa sababu amekuwa akisafiri mara kwa mara na yeye Ommy anasafiri mara kwa mara pia, lakini hakuna bifu lolote kati yao.

  Courtsey:Mdundo

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here