Home Lifestyle Je Ni Kweli ALIKIBA Alimfananisha Msanii RUBY na ‘Ubwa’ ?? RUBY Afunguka...

Je Ni Kweli ALIKIBA Alimfananisha Msanii RUBY na ‘Ubwa’ ?? RUBY Afunguka Ukweli Hapa

Mwezi kama mmoja uliopita, Ruby alijikuta akishambuliwa vikali na mashabiki wa Alikiba baada ya kudai kuwa muimbaji huyo wa ‘Lupela’ alimfananisha na mbwa wakati akihojiwa kwenye kipindi cha The Sporah Show. Tumekaa na Ruby kuzungumza kuhusu suala hilo na amedai kuwa yaliisha.

Ruby

“Ni kwamba bro [Alikiba] hakunikosea chochote, hakuniita mimi mbwa kama inavyosemekana kwa watu kwamba ‘mbwa mbwa’ watu ndiyo wanajaribu kutengeneza beef lakini yule jamaa mimi sina chuki naye na hakuniita hivyo,” amesema Ruby. “Watu wake wa karibu ndiyo watu wanaomfahamu kwahiyo the way walivyoidefine nje huko ilifanya kuleta maana nyingine, iliniletea mimi maana nyingine kwamba bro ulimaanisha hivi nilivyoelewa au ni vile! Kwahiyo mimi nilifanya kama kuuliza lakini sio kumlaumu kwanini, hapana ila ni watu jinsi walivyoupokea,” ameongeza.
“Walitakiwa kusoma kile nilichokiandika ila kwa sababu wamekurupuka siwezi kuwalaumu.” Ruby amesema hana mazoea na Alikiba kwakuwa hawakutani lakini hana tatizo naye na kwamba kama ikitokea wakataka kufanya kazi watafanya tu.
Hata hivyo amesema pamoja na watu kumtukana kwa siku kadhaa mfulilizo, matusi hayakumsumbua chochote.

BONGO5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here