Home Lifestyle “Juma Nature Niache” -KR Muller

“Juma Nature Niache” -KR Muller

Msanii Wa Bongo Flava KR ameyasema hayo alipokuwa akiongea na eNews ya EATV kuhusiana na ushauri aliopewa na rafiki yake ambaye waliimba wote katika kundi la TMK Wanaume family Juma Nature kwamba aangalie asijekulishwa ‘unga’ huko Rader Enteternment ambayo inamilikiwa na msanii TID. Maneno hayo yameonekana dhahiri kumkera KR ambapo hajui kwa nini anaibuka na maneno kama hayo japo kupata ushauri si jambo baya. ”Mimi aniache tuu niendelee na mambo yangu kwani namuheshimu sana na sijui kwa nini amesema mambo yote hayo” Amesema KR. Awali Sir Nature alisema kwamba KR asidanganyike kuitwa Rais huko aliko na akaingia kwenye mtego wa kula unga badala yake atambue kwamba ana familia na ni mtu mzima sasa hivi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here