Home Lifestyle JUX Adai Promota Hawafiki Bei Ndio Maana Haonekani Akifanya Show Nyingi

JUX Adai Promota Hawafiki Bei Ndio Maana Haonekani Akifanya Show Nyingi

Msanii wa muziki wa R&B Juma Jux amesema haonekani akifanya show mara kwa mara kutokana na promota wengi kutofika bei ambayo anahitaji. Muimbaji huyo ambaye aliachia video ya wimbo, One More Night Disemba 10 mwaka jana, amekiambia kipindi cha Sporah Show cha Clouds TV kuwa, mara nyingi amekuwa akipokea simu kutoka kwa mapromota lakini hawafiki kwenye kiwango cha pesa ambacho anahitaji.

juma-jux

“Video zangu nyingi zinarudisha pesa japo sifanyi show nyingi, kwa sababu mimi hata promota wanajua sio kama sipigiwi simu za show, napigiwa simu za show nyingi siyo London hata Tanzania, sema kikwazo ni kiasi changu cha pesa ambacho natakaga, kama unaona ni kikubwa basi namwambiaga promoter nahisi bado sijahit, acha nifanye kazi kwa bidii alafu ukifika muda utanilipa hiyo pesa,” alisema Jux. Aliongeza, “Lakini usinipe milioni 3 au 2 kwa sababu unahisi nahitajika kule, kama unahisi naitajika nilipe milioni 10 au 15. Lakini ukiona hiyo ni nyingi subiri nikaze itafika siku utanilipa hiyo milioni 10. Kwa hiyo hata London ninapigiwa simu, watu wanakwambia kiasi cha pesa ambacho hata nikikaa bongo nakitengeneza,”

Chanzo :Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here