Home Lifestyle “Kiki Linaharibu Muziki, Kwa Sababu Mwisho Wa Siku Watu Hawaangalii Tena Vipaji”-...

“Kiki Linaharibu Muziki, Kwa Sababu Mwisho Wa Siku Watu Hawaangalii Tena Vipaji”- KALA JEREMIAH

Msanii Kala Jeremiah amesema kitendo cha wasanii kuendeleza kiki ili waweze kuzungumziwa kwenye media kuliko kazi zao, kinaua soko la muziki na kuwaharibia kwa mashabiki. Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Kala amesema imefikia hatua sasa wamewabilisha mashabiki, na kufuatilia zaidi skendo zao na sio kazi zao. “Lakini niwe mkweli suala la kiki linaharibu muziki, kwa sababu mwisho wa siku watu hawaangalii tena vipaji, mashabiki tumewabadilisha akili hawashabikii tena muziki, hawashabikii tena kipaji”, alisema Kala Jeremiah.
Pia Kala Jeremiah amesema kulingana na hali hiyo, hata yeye anafikiria kutafuta kiki kabla ya kuachia kazi yake mpya.
“Kweli habari za kiki naziona sana nazisikia, mi mwenyewe nawaza kichwani nipige na demu gani wa bongo movie, tupige pige makiki mawili matatu alafu nitoe goma”, alisema Kala.
Kala aliendelea kusema kuwa kitndo hicho kimeharibu mpaka wasanii wachanga, ambao nao hufikiria kutoka na kiki, ili wajulikane. “Inahamasisha vijana hasa wasanii wachanga, ambao ndio kwanza wametoka, wanaona kama makaka zetu wanafanya hivi kwa nini na mimi nisifanye hivi ili nitoboe, lazima nitoke na kiki, lazima nitoke na kitu fulani ili niongelewe”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here