Home Lifestyle King Kaka Kufunga Ndoa Hivi Karibuni??

King Kaka Kufunga Ndoa Hivi Karibuni??

Baada ya Professor Jay na Mwana FA, kuanga ukapera hatimaye msanii mwingine wa humu nchini huenda akafuata mkondo huo hivi karibuni. Rapper Mkali wa humu nchini KING KAKA ambaye hivi majuzi ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Senzinina’ ametupia picha ya pete mbili huku akiambatisha na maneno “It’s Almost Time…Tick Tock….February 1st”.

king kaka king kaka 2 king kaka 3 king kaka 4

Tulijaribu kumtafuta King Kaka mwenyewe ili aweze kutufafanulia hii kauli ila hakukuwa anapatikana kwa njia ya simu. Mshkaji wake wa karibu ambaye hakutaka tuliweke jina lake wazi alipiga story na MSETO na alikuwa na haya ya kusema “Kaka ni boy wangu sana but when it comes to his personal life yeye huwa private sana though off late amekuwa akinichapia story za harusi, in fact alinishow nitafute suti ya black hadi nikashindwa rada niaje” alisema mshkaji wa karibu wa King Kaka. King Kaka amekuwa katika mahaba kwa muda na mrembo fulani anayejulikana kama NANA, wawili hao wamebarikiwa na Mtoto moja wa kike.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here