“Kuna Msanii Alinikataza Kwenda WCB” -Rich Mavoko

    Msanii Rich Mavoko ambaye sasa hivi yupo chini ya Label ya WCB Wasafi amefunguka na kusema kuwa wakati tetesi za yeye kwenda kujiunga na label ya WCB Wasafi zimeenea kuna msanii mmoja mkubwa wa bongo fleva alimtumia ujumbe na kumwambia anaanzaje kwenda kusimamiwa kazi na msanii Diamond Platnumz. Rich Mavoko amesema hayo hivi majuzi kupitia kipindi cha Planet Bongo na kudai kuwa msanii huyo alimuumiza sana kwa maneno yake hayo ila yeye ilibidi amjibu tu kuwa yeye hafamu ametoka wapi na anakwenda wapi hivyo hawezi kujua mipango ya Mungu kwenye safari yake ya muziki.
    “Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz, kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujae kwangu” alisema Rich Mavoko.

    LEAVE A REPLY

    Please enter your comment!
    Please enter your name here