Home Lifestyle “Kunuka Kwa Viatu Ya MB DOGG,Kilifanya Producer MAJANI Ahairishe Recording Session Yetu”...

“Kunuka Kwa Viatu Ya MB DOGG,Kilifanya Producer MAJANI Ahairishe Recording Session Yetu” -MADEE

Msanii tokea kundi la Tip Top Connection MADEE amefunguka kuwa kunuka kwa viatu ya MB DOGG kilimfanya Producer P FUNK MAJANI ahairishe recording session yao, “Tumeenda kwa mara ya kwanza nimempeleka MB Dog, mi kipindi hiko nishafanya kazi yake Mola kwa hiyo P funk ananielewa vizuri, kufika getini katufumgulia Kajala, sasa kipindi hicho Mb Dog bado yupo rafu sana havai vizuri, tumeingia studio lakini ratiba anaijua Majani kwamba leo hawa machizi wanafanya ngoma, Mb Dog si kavua viatu bwana, ile harufu ambayo ilikuwa inatokea studio, Majani akamind bwana, akawaka utadhani kimetokea sijui kitu gani huwezi amini hatukurekodi siku hiyo, ilibidi Mb Dog atolewe nje tuanze kuoshana oshana miguu, lakini bado mchizi ikawa tayari kashajitoa kwenye mood hatujarekodi”, alisema Madee.
Madee aliendelea kusema kwamba baada ya tukio hilo Majani aliwataka waende siku nyingine, wakiwa wamevaa ndala ili tukio kama hilo lisijitokeze tena, na wakatekeleza ndipo wakarekodi Latifa. MADEE sasa hivi anafanya vizuri na kazi yake mpya ‘Miguli Pande’

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here