Home Lifestyle “Kuoa siyo kigezo cha kushuka Kimuziki” – Mr. Blue

“Kuoa siyo kigezo cha kushuka Kimuziki” – Mr. Blue

Msanii wa Bongo Flava Mr. Blue amesema kuoa siyo kigezo cha kushuka katika utendaji wa mwanamuziki na maisha kwa ujumla kama inavyodhaniwa na watu wengi. Msanii huyo ameyasema hayo katika kipindi cha eNEWS kinachorushwa na kituo cha Eatv ambapo mtangazaji alimuuliza kuhusiana na yeye kuoa na haoni kwamba anaweza kushuka katika kazi zake za sanaa.
Mimi siwezi kufeli kwenye muziki nimepata mitihani mingi kwenye muziki lakini sjashuka hadi leo, nimeanza muziki nikiwa mtoto na sasa hivi nimeshapata mtoto bado nipo kwenye muziki.
”Muziki ni kazi wapo wasanii wengi wa Marekani wameoa lakini wanafanya vizuri , kwa Tanzania mfano Mzee Yusuf ameoa mara mbili lakini sio kwamba ameshuka kwenye game kwa hiyo habari hizi siyo za kweli kabisa”- Amesisitiza Mr. Blue.
Mr. Blue amefunga ndoa hivi karibuni jijini Dar es salaam ambapo kwa sasa ana wawili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here