Msanii wa Bongo fleva Shilole amedai kingereza Kibovu Anachokiongea huwa maksudi, hii ni baada yakuonekana katika mitandaoni mbalimbali ya kijamii akijaribu kwa juhudi zote bila mafanikio kuzungumza lugha hiyo huku ikibaki kuwa kama burudani kwa watu wengine. “Si munaonaga wenyewe muda mwingine nisipoongea kiswangilishi changu watu wanaanza kunitafuta shishi plizi ongea bhana tunataka uongee”,alisema Shilole.