Home Lifestyle Kwa Mara Nyingine Tena Groove Awards Yawatema Nje Bahati Na Willy Paul

Kwa Mara Nyingine Tena Groove Awards Yawatema Nje Bahati Na Willy Paul

Kwa Mara Nyingine Tena Groove Awards Yawatema Nje Bahati Na Willy Paul

Mashabiki wa wasanii wawili wakali wa humu nchini WILLY POZEE na BAHATI,hapo jana usiku walipigwa na alama ya mshangao baada ya kugundua wasanii hao wanaowapenda wametemwa nje kwenye tuzo za Groove Awards 2017.

Bahati na Willy Paul ambao wakati mmoja walidaiwa kuwa na ‘beef’ hawakuwa nominated katika category yeyote katika tuzo hizo zitakozafanyika mapema mwezi ujao, wawili hao wamekuwa wakikashfiwa vikali na baadhi ya mashabiki kuwa nyimbo zao si za ‘Gospel’ ila ni za ki dunia, hata hivyo wawili hao ni miongoni mwa wasanii wanaopendwa sana nchini Kenya.

Wimbo wa Willy Paul na Alaine “I DO” na nyimbo ya Bahati na Rayvanny “Nikumbushe” ni baadhi ya kazi ambazo zinafanya vizuri sasa hivi humu nchini, Kazi ya Msanii Mr Seed ambayo amemshirikisha Bahati “Kumbe Kumbe” pia haikuweza kuteuliwa katika nominations za tuzo hizo zilifonyika hapo jana.

Walioteuliwa katika category ya Best Male Artiste ni Kriss Erroh, Daddy Owen, Pitson, Eko Dydda, Pastor Anthony Musembi na Guardian Angel huku Best Female Artiste nayo ikibeba Alice Kimanzi, Size 8, Princess Farida, Kambua, Mercy Masika na Evelyn Wanjiru.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here