Home Lifestyle Lady Jaydee kutoa kauli yake leo baada ya kudai kudhalilishwa na Gardner

Lady Jaydee kutoa kauli yake leo baada ya kudai kudhalilishwa na Gardner

Siku 14 tangu Mtangazaji wa Clouds Fm Gardner Habash kudaiwa kutoa lugha ya udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mke wake Judith Wambura, mwanamuziki huyo maarufu kwa jina la Lady Jaydee, amesema leo anatarajia kutoa tamko rasmi kuhusu suala hilo.
“Nipo katika maandalizi ya tamasha langu ndiyo maana ilikuwa vigumu kwangu kulizungumzia hili, Jumatatu (leo) nitatoa tamko,” alisema Jaydee. Mei 13 kupitia mwanasheria wake Amani Tenga kutoka kampuni ya Law Associates Advocate, alimwandikia barua ya kumtaka mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner Habash kuomba radhi mbele ya umma ndani ya siku 7 kwa kauli ya udhalilishaji aliyoitoa dhidi yake.

Gardener JAY DEE
Gardner anadaiwa kutamka maneno ya udhalilishaji dhidi ya Jaydee Mei 6 mwaka huu na kurekodiwa kisha video kusambazwa katika mitandao ya kijamii, katika ukumbi wa CDS PARK (zamani TCC) alipokuwa akisherehesha tamasha la Miss TIA 2016, Taarifa iliyosomeka katika barua hiyo ya mwanasheria ilimtaka Gardner aombe radhi na iwapo akikaidi, akishindwa au kuzembea ndani ya siku saba, atachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi ya udhalilishaji na kashfa. Mwananchi lilimtafuta Gardner na kumuuliza iwapo amepokea barua hiyo na matarajio yake ya kujibu tuhuma zinazomkabili, lakini mtangazaji huyo alikaa kimya kwa muda wa sekunde 10 na baadaye alisema; “sina maoni yoyote kuhusu jambo hili.” Barua iliyoandikwa na mwanasheria huyo ilisomeka kuwa kauli ya Gardner, maneno yake hayo yalikuwa yanamhusu Jaydee moja kwa moja hivyo kusababisha udhalilishaji mbele ya umma.

Source:Mwananchi/Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here