Home Lifestyle Linex Awachana Wasanii Wanaotaka Kutoboa Afrika

Linex Awachana Wasanii Wanaotaka Kutoboa Afrika

Msanii Linex Mjeda amefunguka na kuwachana baadhi ya wasanii ambao wanataka kutoboa kimataifa na kuhangaika na soko la kimataifa wakati wasanii hao hawajaweza kulishika vizuri soko la Afrika Mashariki. Linex alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio na kusema kuwa yeye kwa sasa anapigana na soko la Afrika Mashariki kwanza maana anaamini kuna wasanii wengi wanahangaika na soko la kimataifa na Afrika wakati bado hawana uwezo wa kufanya show nchi jirani kama Kenya, Uganda, Rwanda na kwingineko sababu bado hawajaweza kufanikiwa kutoboa katika soko hilo la Afrika Mashariki. “Wasanii wengi wametolea macho soko la kimataifa, wakati Kenya yenyewe hawana uwezo wa kufanya show, mimi saizi lengo langu ni kujiuza katika soko la Afrika Mashariki, sasa ni soko gani la Afrika unatafuta wakati nchi jirani hapo tu Kenya huna uwezo wa kupiga show, halafu unakaa unaniambia unatafuta soko la Kimataifa, market gani unatafuta wewe kama Kenya huwezi kufanya show, Burundi huna uwezo wa kufanya show, Rwanda sijui huna hata mtu”. Linex ameendelea kusema “Mimi nimekaa Kenya wiki mbili tatu nimesanuka kuwa wasanii wa bongo wenye uwezo wa kufanya show Kenya hapo hawazidi hata kumi. Sasa hilo soko la Kimataifa unalolitafuta ni lipi wakati Kenya hapo watu hawakujui? Kwa hiyo mimi mwaka huu na mwakani lengo langu ni kutafuta soko la Afrika Mashariki tu” alisema Linex.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here