Kupitia kipindi cha Planet Bongo MADEE Ameka Wazi Kuhusu issue ya Kufumaniwa Na SHILOLE na Kusema kuwa swala hilo halina ukweli wowote na kudai kuwa Shilole ni rafiki yake ambaye mara kadhaa walikuwa wakitembeleana kwa ajili ya kusalimiana na kupanga mipango mingine ila hakuwahi kutoka na naye kimapenzi na wala hajawahi kufumaniwa na Nuh Mziwanda kama ambavyo inasemekana. ” Siyo kweli Shilole ni rafiki yangu kama marafiki wengine, labda huyo Nuh Mziwanda angeleza vizuri aliwahi kunifumania wapi, lini na wakati gani labda naweza kukumbuka lakini ukweli ni kwamba yule ni rafiki yangu kama walivyo rafiki wengine hivyo naomba ieleweke hivyo” alisema Madee.