Home Lifestyle “Mambo ya ALIKIBA na DIAMOND ni Siasa ya Tanzania, Hatuoni Shida Kufanya...

“Mambo ya ALIKIBA na DIAMOND ni Siasa ya Tanzania, Hatuoni Shida Kufanya Nao Kazi Wote – SAUTI SOL

Member wa kundi la Sauti Sol, Savara amesema kufanya kazi na Alikiba haimaanishi kuwa wanamkubali zaidi kuliko Diamond. Kundi hilo lilifanya wimbo Unconditionally Bae na Alikiba uliofanya vizuri. “Mambo ya Alikiba na Diamond hiyo ni siasa ya Tanzania,” member wa kundi hilo, Savara amekiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka aliyeuliza iwapo kundi hilo linaona kuwa uimbaji wa Alikiba unaendana zaidi na mtindo wao kuliko wa Diamond.“Mimi ni msanii, yule ambaye anakuja wa kwanza na yule ninayefeel vibe yake nitafanya naye muziki, muziki utafanywa kila siku, haijalishwi unafanya na nani, mimi nitafanya hata collabo na Diamond, tutafanya collabo na msanii mwingine yeyote,” amesema. Pia Savara amesema watafanya wimbo na Vanessa Mdee huku wakipenda pia kumtumia Nahreel siku za usoni kushiriki kutengeneza nyimbo zao. Lakini pia amedai kuwa ametengeneza wimbo wa Joh Makini.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here