Home Lifestyle MB DOGG Kuachia Video Mpya Ya Wimbo ‘Uwe Wangu’ aliyoshoot IRELAND

MB DOGG Kuachia Video Mpya Ya Wimbo ‘Uwe Wangu’ aliyoshoot IRELAND

Msanii kutoka ‘label’ ya QS Mhonda, MB Dog anatarajia kuachia video mpya ya wimbo ‘Uwe Wangu’ kama zawadi ya msimu huu wa sikukuu ya Valentine Day.
Muimbaji huyo ambaye aliachia video ya wimbo ‘Sio Siri’ hivi karibuni, ameiambia Bongo5 kuwa ameamua kuachia kazi hiyo aliyoshoot katika visiwa vya Ireland kama zawadi kwa mashabiki wake.
“Mashabiki wanataka muziki mzuri kila siku bila kujali unatoa ngoma ngapi. Kwahiyo hii ‘Uwe Wangu’ ni kama zawadi kwa mashabiki wangu, video ameshoot na Abby Kazi katika visiwa vya Ireland,” alisema MB Dog. Pia MB Dog amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani ana mzigo wakutosha kwa ajili ya mashabiki wake.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here