Home Lifestyle “Mimi sijaumbwa kwa ajili ya kuchezea wanawake” – Harmonize

“Mimi sijaumbwa kwa ajili ya kuchezea wanawake” – Harmonize

Mkali wa wimbo ‘Bado’ kutoka WCB, Harmonize amesema hana tabia ya kuchezea wanawake hivyo kama wakikubaliana na mpenzi wake wa sasa Jacqueline Wolper watafunga ndoa. Muimbaji huyo ambaye ametoka katika familia ya dini ya kiislamu, ameiambia Bongo5 kuwa dini yake hamruhusu kuwachezea watoto wa kike. “Kwa sasa kuweka wazi kama tunakaa pamoja au hatukia siyo kitu kizuri cha kuzungumzia kwa sasa,” alisema Harmonize. “Insha’Allah panapo majaliwa tutakaa pamoja kwa sababu mimi sijaumbwa kwa ajili ya kuchezea wanawake,”
Aliongeza, “Nikiwa na mwanamke tunaandaa future, tunakubalia tukae pamoja, kwa nini tusikae pamoja wakati dini yangu hainkruhusu,”
Harmo amewataka mashabiki wa muziki wake kutulia kwani kuna mambo yazuri yanakuja.

Bongo5

5 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here