Home Lifestyle Mose Iyobo: Mimi na Aunt tupo sawa, akanusha Aunt Ezekiel Kuchepuka

Mose Iyobo: Mimi na Aunt tupo sawa, akanusha Aunt Ezekiel Kuchepuka

Baada ya kuzagaa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuwa dansa wa Diamond, Mose Iyobo na mama mtoto wake Aunt Ezekiel, wameachana na kila mtu anaishi kwake, Mose amefunguka na kusema mahusiano yao yapo salama kabisa. Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Mose alisema habari za kwamba ameachana na Aunt Ezekieli kisa Aunt amechepuka sio za kweli. “Hivi vitu naviona na najua ni vitu vya kuzusha tu, mimi na mama Cookie tupo vizuri na hatuja kwaruzana. Kwa hiyo hivyo vitu sio vya kweli na wala hatujaachana,” alisema Mose. “Kugombana tunagombana, ni vitu vidogo vigogo vya ndani ya nyumba. Pia nilisikia sisi tumeachana kila mtu anaishi kwake, sio kweli, kipindi hicho mimi nilisafiri sasa walivyokuwa wanamuona yupo peke yake, ndio wakazusha hivyo,” aliongeza. Mose amesema hizi tetesi hazimuumizi kichwa kwa kuwa tayari anajua sio vitu vya kweli.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here