Home Lifestyle Msanii Tunda Man Apata Ajali Mbaya Ya Barabarani Huku Dereva Wake...

Msanii Tunda Man Apata Ajali Mbaya Ya Barabarani Huku Dereva Wake Akiaga Dunia. (Habari zaidi)

Msanii Tunda Man amepata ajali mbaya ya gari pamoja na wenzake watano wakilipokuwa wakitoka show Eneo la Idetelo, katikati ya Nyololo na Makambako  huku dereva akifariki papo hapo.

Haya ndiyo Tunda alisema baada ya mkasa huo mbaya.

”‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki

Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo.

(Picha Kwa Hisani Ya MilardAyo.com)

4flkp 7flkp (1) 9flkp

Utakumbuka kwamba mwaka wa elfu mbili na kumi na moja pia Tunda alihusika katika ajali nyingine ya barabarani ambayo ilipelekea dereva wake kupoteza maisha yake  wakiwa safarini kutoka Kahama wakielekea Shinyanga.

Pole sana Tunda man kwa ajali na kumpoteza dereva wako.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here