Home Lifestyle Mwanamziki Mkongwe Nchini Tanzania Babu Seya kukimbilia Mahakama ya Haki za Binadamu...

Mwanamziki Mkongwe Nchini Tanzania Babu Seya kukimbilia Mahakama ya Haki za Binadamu na Watu ya Afrika!

MWANAMUZIKI mkongwe nchini Tanzania , Nguza Viking anayejulikana sana kwa jina la  ‘Babu Seya’ anayetumikia kifungo cha maisha jela na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa kuwanajisi watoto tisa sasa wameammua kuelekea mahaka ya Haki za Binadamu na Watu ya Afrika (AFCPHR), baada ya kushindwa katika mahakama kuu nchini Tanzania. Wanamziki hao walifungwa mwaka wa Elfu mbili na Nne kutumikia kifungo cha maisha gerezani.

nguza-viking-nov22-2013

Utakumbuka kwamba wawili hao pamojana jamaa  mwingine mmoja  kwa jina la Mwalimu walishtakiwa kwa tuhuma  kumi za unajisi.Babu seya walipatikana na makosa ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa,   Sinza   Dar es Salaam. Kwa sasa tuungoje uamuzi wa mahakama ya Haki za Binadamu na Watu ya Afrika (AFCPHR),kesi ambayo itang’oa nanga Machi Kumi na moja mwaka huu.Kwa maoni yako, Babu seya na wenzake waendelee kutumikia kifungo chao cha maisha ama sheria ichukue mkondo wake?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here