Home Lifestyle ‘Namuombea JACK PATRICK Atoke Jela Mapema’ – Asema VANESSA VANESSA MDEE ;...

‘Namuombea JACK PATRICK Atoke Jela Mapema’ – Asema VANESSA VANESSA MDEE ; JACK PATRICK Ni Ex Wa JUX

Vanessa Mdee amesema anamuombea Jack Patrick atoke jela mapema. Jack aliyefungwa jela nchini China baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aliwahi kuwa mpenzi wa Jux, ambaye kwa sasa ni boyfriend wa muimbaji huyo wa Niroge.
“Namuombea atoke jela mapema, nadhani matatizo anayoyapata kule ni makubwa kuliko haya ambayo tunafiria sisi,” ameiambia Global TV.
“Sidhani hata kama huwa ananifikiria, nadhani anafikiria familia yake na hali ambayo anakosa maisha ya kawaida,” aliongeza.
Vanessa aliyeachia wimbo mpya Niroge hivi karibuni alisisitiza kuwa hakumuibia Jack bwana (Jux) na kwamba alikuwa akimfahamu msichana huyo kama model wengine.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here