Home Lifestyle Naomba SHETTA Usinirudishe Enzi Za MR NICE – DUDU BAYA

Naomba SHETTA Usinirudishe Enzi Za MR NICE – DUDU BAYA

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Dudu Baya amemtaka Shetta kuacha kutumia jina la ‘Mamba’ kwani hiyo ni ‘aka’ yake ambayo amekuwa akiitumia kwa miaka mingi. Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Dudu Baya alisema anaomba Shetta aache mara moja kutumia jina hilo ili yasije yakatokea kama ya Mr Nice. “Shetta ni kama mdogo wangu sitaki ugomvi nae, asinirudishe enzi za Mr Nice,” alisema “Mbona majina yapo mengi kwanini atumie jina langu (Mamba). Naomba afikishiwe huu ujumbe, nimemtafuta kwenye simu hapatikani,” alisema Dudu Baya. Dudu Baya amedai ameona mara kadhaa msanii huyo anatumia jina lake bila kuongea nae.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here