Home Lifestyle “Natamani Sana Kuimba Gospel Kama Zamani” – RUBY

“Natamani Sana Kuimba Gospel Kama Zamani” – RUBY

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania RUBY ambaye alianza kuimba muziki kupitia kanisani kwenye kwaya amefunguka na kusema kuwa kuna baadhi ya makanisa Tanzani hata ukiingia ndani unahisi unafiki moja kwa moja. Ruby akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio alisema yapo baadhi ya makanisa ukiingia ndani unaona kweli uwepo wa Mungu ndani yake na kusema lakini yapo makanisa mengine ukiingia unaona unafiki wa hali ya juu.
“Unajua mimi nafanya muzuki huu wa bongo fleva kama kazi hivyo hata watu wanatakiwa kuelewa hii ni kazi yangu kama ambavyo wao wanakwenda kazini Jumatatu mpaka Ijumaa na mimi ndiyo hivyo hivyo, hivyo kuna wakati mwenyewe natamani sana kuimba gospel ila nabaki naimba moyoni ila nime miss kuimba mbele ya watu kama zamani nikiwa kanisani” alisema Rubby
Mtangazaji alitaka kufahamu kama msanii huyo alishawahi kuitwa kutoa huduma kwenye kanisa lolote lile kama muimbaji wa nyimbo za injili ndipo alipofunguka na kusema kuna makanisa mengi sana yapo kinafiki hata ukiingia ndani una fell unafiki na hakuna uwepo wake Mungu na kusema yapo makanisa machache sana ambayo ukiingia hata ndani una fell uwepo wake Mungu.
Mbali na hilo msani huyo amesema kuwa kwa sasa anajipanga kuachia Album yake ya kwanza hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here