Home Lifestyle Navy Kenzo Wala Bonge La Shavu

Navy Kenzo Wala Bonge La Shavu

Ni  Headlines za kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Nahreel na Aika limechaguliwa kuwa mabalozi wapya wa Application ya simu iitwayo Klobaa inayohusika kuwakutanisha watumiaji wa hiyo application hiyo sehemu  mbalimbali za burudani nyakati za usiku kamaClubs na Lounges pamoja na matukio mbalimbali..Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Aika alisema…’Hawa wamekuwa wakitutafuta tangu mwaka 2015 hili shavu tulikuwa tunazungumza nao kwahiyo mwisho wa siku tukakubaliana na tukapewa ubalozi kwahiyo watakuwa wakitutumia sisi kama kutangaza Application yao, tumesaini nao mkataba wa miaka miwili‘- Aika. ‘Kazi yangu sisi ni kusafiri nao wanatuonyesha jinsi ya watu wanavyostarehe katika Clubs, Lounges pia kutangaza kazi zetu za muziki kupitia shavu hili tutaenda nao Marekani, Dubai, South Africa na nchi nyingine kuitangaza hii Application yao mpya tukiwa na kazi zetu– Aika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here